Kongamano la 37 la Chama cha wanafunzi wa Kiswahili Afrika Mashariki (Chawakama) limefanyika katika chuo kikuu cha Chuka tarehe ya 4 Novemba, 2023. Kongamano hilo lilihusisha vyama vya taaluma ya Kiswahili kutoka vyuo vikuu mbali mbali vya kanda ya Afrika Mashariki kama vile Chakichu, Chakikemu na kadhalika. Wageni mashihuri walikuwa Dkt. James Ontieri na mlezi wa Chawakama, Dkt. Sheila Wandera.
Naibu Makamu wa Chansela, Prof. Gilbert Nduru, alifungua rasmi kongamano hilo. Wengine waliohudhuria ni pamoja na mtiva wa kitivo cha sanaa na sayansi ya jamii Dkt. Christopher Kiboro, mlezi wa Chakicha Dkt. Allan Mugambi, mkuu wa kitengo cha Kiswahili CU, Dkt. Dorcas Musyimi pamoja na wahadhiri wengine kutoka vyuo vikuu mbali mbali kama Nairobi, Egerton, Rongo, Kaimosi, Tharaka, Embu, Kenyatta, Karatina, miongoni mwa wengine.